Tokea kugundulika kwa teknolojia ya mawasiliano(internet) imeenda kubadilisha nyanja mbalimbali ya maisha yetu. Jinsi tunavyowasiliana na marafiki, tunavyopata taarifa, jinsi tunavyo burudika na miziki na filamu na hatimaye pia jinsi tunavyo fanya manunuzi ya bidhaa mbalimbali.
Kwa mujibu wa taarifa Tanzania hadi ilipofikia Januari 2021 ilikuwa na watumiaji wa intaneti takribani millioni 15 na kati ya vipao mbele vya Rais wa Tanzania wa awamu ya sita, Muheshimiwa Samia Suluhu Hassan, watumiaji wa intaneti nchini inatazamiwa kuongeza hadi kufikia asilimia 80 ya watanzania mwaka 2025.
Hili ni jambo jema na litaleta manufaa makubwa katika ufanyaji biashara mtandaoni na kusaidia kupunguza changamoto zilizokuwa zikiikabili sekta hii.
Kimsingi zipo faida nyingi katika ununuzi wa bidhaa kwa njia ya mtandao zinazolenga katika kumnufaisha mteja zaidi tofauti na maduka ya kawaida tuliyoyazoea. Faida hizi ni kama zifuatazo
Faida 5 Kubwa Za Manunuzi Mtandaoni
Urahisi Wa Manunuzi
Kati ya faida kubwa kuliko ya kununua bidhaa na huduma mtandaoni ni urahisi wake wa kutafuta na kupata kile unachokihitaji. Hakuna haja ya kwenda dukani na kupanga mstari kungoja kuhudumiwa, unaweza kufanya manunuzi yako kokote ulipo ukiwa na kifaa chako simu au kompyuta iliyounganishwa na huduma ya intaneti. Pia unaweza kufanya manunuzi saa yoyote na siku yoyote ile kwani duka la mtandaoni lipo wazi siku saba za wiki masaa ishirini na nne.
Bei Poa
Hakuna mahala utakapoweza kupata bei nzuri ya bidhaa na huduma kuzidi maduka ya mtandaoni. Sababu kuu ni kwamba maduka mengi ya mtandaoni ( kama la kwetu) hununua bidhaa zake za kuuza moja kwa moja toka kiwandani na hivyo kuondoa gharama za mtu wa kati na kuweza kukupatia wew mteja bei nzuri zaidi. Pia ukilinganisha na gharama za uendeshaji za duka la mtandao liko chini ukilinganisha na maduka ya kawaida ambayo yanatakiwa kulipa gharama za kodi, wafanyakazi,umeme, usafi na kadhali; haya yote hupelekea maduka hayo kuuza bidhaa na huduma zake kwa bei ya juu.
Bidhaa Nyingi Za Aina Tofauti
Maduka ya mtandaoni kwa mara nyingi yamesheheni bidhaa mbalimbali za makampuni tofauti tofauti. Hii hukupa machaguo mengi sehemu moja na hakuna haya kuzunguka kutafuta kitu kimoja kimoja.Utapata bidhaa ya aina moja iliyotolewa na makampuni tofauti, hii inakupa nafasi kulinganisha bidhaa kampuni kwa kampuni na kufanya manunuzi mzuri wa kujirishisha.
Kununua Na Kutuma Zawadi Kwa Uwapendao Kwa Urahisi.
Njia rahisi ya kutuma zawadi kwa wapendwa wako kwenye matukio mbalimbali kama sherehe ya kuzaliwa, siku ya wapendanao au siku kuu, ni kupitia maduka ya mtandao. Kufungasha zawadi na kumpelekea muhusika hilo jukumu hufanywa na maduka la mtandaoni pale tu ukishamaliza maliza malipo na kuacha maelekezo ya muhusika wa zawadi.
Mapunguzo Ya Bei Na Promosheni Mbali Mbali
Maduka ya mtandaoni mara kwa mara huendesha mapunguzo makubwa ya bei na pia promosheni mbali mbali kama vile nunua kimoja upate kingine bure (buy one get one free); kupata pointi kila ununuapo bidhaa na ukaweza kubadili pointi hizo kuwa punguzo la bei; kuponi za pungozo la bei kwa matukio maalumu kama vile kununua bidhaa yako ya kwanza, siku yako ya zaliwa, siku yako uliojiandikisha kwenye tovuti na kadhalika. Zote hizi humnufaisha mnunuaji kwa kupata bei nzuri kabisa katika manunuzi yake.
Hizo ni baadhi tu ya faida unazoweza kuzipata kwa kununua mtandaoni na hasa kutoka tovuti yetu ambapo tumejizatiti kukurahishia manunuzi yako katika ubora na usalama zaidi.
Tuambie je ushawahi kujaribu kufanya manunuzi kwenye mtandao? Changamoto gani ulizipata? Je ni faida ipi inayokuvutia zaidi kutaka kufanya manunuzi katika mtandao?
Habari Bruno, bidhaa nyingine nyingi zinaongezwa kadiri ya uwezo wetu kwa sasa. Dhumuni letu ni kuja kuwa na bidhaa zaidi ya 1000 tofauti. Endelea kuwa nasi, karibu sana!
Habari Bruno, ukitaka mzigo utumwe kwako kama ni nje ya Dodoma mjini unapaswa kufanya malipo kwanza ndio mzigo utumwe.
Kama upo maeneo ya Dodoma mjini basi una option ya kuletewa ulipo ndio ufanye malipo ama ukafika dukani kwetu na kufanya malipo na kuchukua mzigo wako.
12 comments on “FAIDA ZA KUNUNUA BIDHAA MTANDAONI”
Chifuu
Point namba 1 na 4 ndizo zinanifanya nipende online shopping
Samuel Makalla
Naam, hakika online shopping imerahisisha maisha sana.
Heriekay
Sikuwa mtumiaji wa mtandao katika ununuzi wa bidhaa ila nmejifunza na kuona umuhimu na uzuri wake kutoka kwako
Samuel Makalla
Nafurahi kusikia hivyo, karibu kwenye ulimwengu mpya wa manunuzi yenye faida zaidi kwako.
Bruno.Albogast
Nimeipenda kwakweli but naona bidhaa nyingi akuna boss ?
Samuel Makalla
Habari Bruno, bidhaa nyingine nyingi zinaongezwa kadiri ya uwezo wetu kwa sasa. Dhumuni letu ni kuja kuwa na bidhaa zaidi ya 1000 tofauti. Endelea kuwa nasi, karibu sana!
Bruno.Albogast
Nimeipenda kwakweli but naona bidhaa nyingi akuna boss ?
Bruno.Albogast
Sijajua ukinunua bidhaa malipounafanya bahada yakupata bidhaa au kabla ya kupata bidhaa?
Bruno.Albogast
Sijajua ukinunua bidhaa malipounafanya bahada yakupata bidhaa au kabla ya kupata bidhaa?
Samuel Makalla
Habari Bruno, ukitaka mzigo utumwe kwako kama ni nje ya Dodoma mjini unapaswa kufanya malipo kwanza ndio mzigo utumwe.
Kama upo maeneo ya Dodoma mjini basi una option ya kuletewa ulipo ndio ufanye malipo ama ukafika dukani kwetu na kufanya malipo na kuchukua mzigo wako.
Bruno.Albogast
Natatafuta hii bidhaa boss wngu HUAWEI SOUND JOY please helpe me
Samuel Makalla
Habari Bruno, bidhaa hiyo hatuna kwa sasa. Tafadhali endelea kuwa nasi, karibu!